JIMBO KATOLIKI SUMBAWANGA

WANAWAKE WAKATOLIKI TANZANIA
(WAWATA)

HISTORIA NA WAASISI WA WAWATA NDANI YA JIMBO

RASMI UTUME HUU WA AKINA MAMA WAKATOLIKI ULIANZA ANDANI YA JIMBO LA SUMBAWANGA MNAMO MWAKA- 1972

 1. WAANZILISHI WA WAWATA JIMBO LA SUMBAWANGA
  TERESIA KITUPI — MWENYEKITI
 2. TASIANA MAKUNGU – MAKAMU MWENYEKITI
 3. ROMANA MAUFI – KATIBU
 4. ODETHA MAZWILE – KATIBU
 5.  JOSEPHINA SIAME – MHASIBU

Utangulizi

3. UTUME WETU:
– kuwawezesha akina mama kuwa na mtazamo wa Maendeleo ya kiuchumi
Kuwaunganisha Wanawake Wakatoliki Tanzania
kuunganisha Wanawake waweze kushiriki katika kujenga familia bora zaKikristo.
Kushiriki na Wanawake Wakatoliki kama Kiungo ( WUCWO ) Word Union of
Catholic Womens Organizations, ili kujenga dunia yenye Usawa Haki na Amani.
Kuwawezesha Wawata Kushiriki vikao vya ngazi zote ndani ya Kanisa.

MAMA. MARGARET RAINERY

-Mwenyeki wa WAWATA Jimbo Sumbawanga.
Tukiwa katika Hija ya Kijimbo Parokia ya Chala.

4.  MAFANIKIO MPAKA SASA:

 • Tumefanikiwa kujitakatifuza kwa njia ya mafungo, sala na tafakari
  mbalimbali.
 • Tumefanikiwa kufanya semina mbalimbali katika Parokia zetu Kiroho
  na Kimwili
 • Tumefanikiwa kuwaunganisha Kijimbo.
 • Tumefanikiwa kuwapa elimu ya Miradi katika kutoa mikopo yenye tija,na elimu
  ya Afya kwa Wanawake. Lishe bora, na Malezi ya watoto.
 • Tumefanikiwa kuwaimarisha Wana WAWATA kiuchumi katika ngazi yakaya.
 • Tumefanikiwa kuwa na siku maalumu ya kutembelea KAENGESA MAMA
  DAY ikiwa ni pamoja na Kulea Miito na kutegemeza Seminari yetu Jimboni
  Sumbawanga.
 • Tumefanikiwa kutoa matendo ya Huruma kwa wahitaji katika jamii yetu.
 • Akina Mama wameweza kujitambua katika Parokia zetu 27 za Jimbo.
 • Tumefanikiwa kushiriki vikao Jimbo, Kanda hadi Taifa.
 • Tumefanikiwa kuwa na shamba la ekari saba ambalo limepandwa miti na
  tunaendelea kupanda miti.
WAWATA 3
Shamba la Miti
WAWATA 4
WAWATA 5
Tumefanikiwa kuzindua Proggram ya WAWATA chipukizi.

5. MALENGO:
Kuwaunganisha Wanawake Jimboni katika Juhudi zao zinazowahusu kama
Wakristo Wanawake, na raia, wakiwa katika vikundi mbalimbali ambavyo hasa
lengo lao ni kulistawisha Kanisa na jamii.

 • Kuwahamasisha Wanawake ili waweze kushirikiana na waamini wote katika kujenga
  familia bora za Kikristo popote Jimboni.
 • Kuwatia moyo Wanawake Wakatoliki katika Kujiendeleza na kujitambua hadhi yao, kama
  Wanawake katika Kanisa ili waweze kutimiza wajibu wao kikamilifu kama waamini wote
  wanavyotakiwa tukiongozwa na kauli mbiuyetu ya -KWA UPENDO WA KRISTU,
  TUTUMIKIE NA KUWAJIBIKA.
 • Kuhimiza Wanawake Wakatoliki wote kushiriki na kujiunga na Wanawake wakatoliki Jimboni kwa kuzingatia maadili ya Kanisa Katoliki.
 • Kushiriki na Wanawake Wakatoliki wa dunia kama kiungo cha WUCWO ili kujenga dunia yenye usawa, haki na Amani.
 • Kuwaelimisha na kuwahimiza Wawata kwa kila njia ili wawe na uwezo wakushiriki kikamilifu pamoja na Wanawake wote Tanzania katika shughuli zote za maendeleo ya Wanawake na kwa ujumla. Kiuchumi, Kisiasa, pia kujiunga katika mashirika na vyama mbalimbali vya Wanawake Nchini visivyopingana na maadili ya Kanisa Katoliki.
 • Kuwawezesha Wanawake Wakatoliki Jimboni kuwakilisha katika vikao mbalimbali vya WAWATA Kanisa, Halmashauri ya Walei kwa ujumla katika Maendeleo mbalimbali.

6. VIONGOZI WA WAWATA NGAZI YA JIMBO.
1996 – 2010

 1. JOSEPHA MICHESE – MWENYEKITI
 2. ASILA SAWILO – MAKAMU MWENYEKITI
 3. ROSE MCHUNGUZI – KATIBU
 4. TERESIA SUWIKASAMIA KATIBU MSAIDIZI
 5. JOSEPHINA SIAME – MHASIBU

2011-2022

 1. SARAPHINA SULEIMAN – MWENYEKITI
 2. SCHOLASTIKA LAZARO – MAKAMU MWENYEKITI
 3. ROZALIA MWANAKULYA – KATIBU
 4. EMMY VICTOR – KATIBU MSAIDIZI
 5. TERESIA MASHAURI – MHASIBU

2022-2026

 1. MAGRETH LUKALA – MWENYEKITI
 2. SCHOLASTIKA LAZARO – MAKAMU MWENYEKITI
 3. EMMY VICTOR – KATIBU
 4. MARIETHA MLWILO – KATIBU MSAIDIZI
 5. EVELINA JAIROS – MHASIBU

PICHA MBALIMBALI ZA WANAWAKE WAKATOLIKI JIMBO LA SUMBAWANGA.

small efforts make big change