Mapokezi ya Mwadhama Polycarp Kardinal Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki Dsm, alipowasili Jimbo Katoliki Shinyanga katika ziara za kichungaji, mnamo tarehe 6.12.2023.
Katika picha ni baadhi ya waamini wa jimbo katoliki la Shinyanga wakiwa na nyuso za furaha wakimkaribisha Kardinali Pengo katika mipaka ya jimbo hilo
Mha Askofu Sangu aongoza mapokezi na kumkaribisha Mwadhama kadinali Pengo jimboni humo kwa ziara ya kichungaji kuanzia tar 06.12.2023
Sherehe ya Bikira Maria Kupashwa Habari kuwa atakuwa ni Mama wa Mungu kwa mwaka 2024 inaadhimishwa Jumatatu tarehe 8 Aprili 2024, baada ya tarehe 25 Machi 2024 kuangukia kwenye Juma Kuu. Tarehe 8 Aprili 2024 Mama Kanisa sehemu mbalimbali za dunia anaadhimisha Siku ya Kutetea Uhai na Utakatifu wa Maisha tangu pale mtoto anapotungwa mimba…
Dominika ya Sita Ya Mwaka B wa Kanisa: Siku ya 32 ya Wagonjwa Ulimwenguni 2024 Maadhimisho ya Siku ya 32 ya Wagonjwa Ulimwenguni yananogeshwa na kauli mbiu “Si vizuri kwamba mwanadamu awe peke yake. Uponyaji wa wagonjwa katika kuponya mahusiano.” Baba Mtakatifu anaangalia vita kama gonjwa kubwa na la kutisha, uzee na upweke. Kumbe, kuna…
Ufufuko wa Kristo Yesu ni kilele cha ukweli wa imani ya Kikristo, ambayo jamii ya kwanza ya wakristo iliusadiki na kuuishi kama kiini cha ukweli. (SumbawangaMedia) Na. Padre Joseph Herman Luwela-Kutoka Vatican Rome Ufufuko wa Kristo Yesu ni kilele cha ukweli wa imani ya Kikristo, ambayo jamii ya kwanza ya wakristo iliusadiki na kuuishi kama…
Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu. Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu? Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako..”( Zaburi 42:1 – 3 )
Na Padre Joseph Herman Luwela, – Vatican. Nyumba ya Baba yangu ni nyumba ya sala, toba na wongofu wa ndani na sio genge la biashara huria! Leo Kanisa linaadhimisha Dominika ya 3 ya Kipindi cha Kwaresima Mwaka B wa Kanisa. Himizo kubwa katika kipindi hiki cha Kwaresima ni toba na wongofu wa moyo na muunganiko…
Kipindi cha Kwaresima ni fursa ya kuamsha na kupyaisha ari na mwamko wa kimisionari, tayari kujisadaka bila ya kujibakiza kwa ajili ya kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu hadi miisho ya dunia. Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waamini kuwakumbuka na kuwaombea wainjilishaji wote, ili waweze kuwa ni vyombo na mashuhuda wa kile wanacho amini, kufundisha…