Tarehe 07.12.2023 mwaka wa Bwana katika nyumba ya malezi parokia ya Chala
Katika picha ni Masista 16 wa nadhiri za kwanza wa shirika la Maria Mtakatifu Malkia wa Afrika-Jimbo la Sumbawanga 07.12,2023
Adhimisho la Misa Takatifu limefanyika katika Kanisa la Nyumba ya malezi ya Shirika hilo, iliyopo Parokia ya Mtakatifu Fransisco wa Sales – Chala Jimbo Katoliki Sumbawanga. Ikiwa ni utangulizi wa sherehe za Shirika hilo, ambazo hufanyika tarehe 08.12. au maarufu Nane Disemba Sherehe ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi(Emakulata).
Adhimisho la Misa Takatifu limeongozwa na Askofu Emeritus Damian Kyaruzi wa Jimbo la Sumbawanga, Na aliyepokea Nadhiri 16 za kwanza kwa Masista 16 ni Mama Mkuu wa Shirika hilo Mheshimiwa SR. Editruda Mbegu Mbele ya Mhashamu Baba Askofu Damian Kyaruzi, ambaye amemwakilisha askofu wa Jimbo Mha, Beatus Urassa ALCP/OSS.
Katika sherehe hizo za nadhiri za kwwanza wameudhuria , watu mbalimbali wakiwemo mapadri, watawa waamini wakinogeshwa na furaha ya walelewa amabo wameshuhudia safari ya dada zao ikifika mwisho katika hatua msingi ya nadhiri za awali tunawaombea udumifu mwema
Katika picha hapo chini ni mnadhiri mpya wa nadhiri za kwanza Sista Maria Nzunda kutoka parokia ya Tunduma jimbo katoliki Sumbawanga
Na. Pd Joseph Luwela-Vatican-Roma Utakatifu ni mchakato unaowawezesha waamini kuishi upendo katika utimilifu wake kadiri ya nguvu na mwanga wa Roho Mtakatifu. Maisha ya kila mwamini yawe ni kielelezo cha utume kutoka kwa Kristo Yesu anayetaka kuwaletea waja wake mabadiliko katika maisha, licha ya udhaifu na mapungufu yao ya kibinadamu, daima wakijitahidi kuambata upendo wa…
Na Padre Joseph Herman Luwela, – Vatican 06.Jan 2024 Mamajusi toka mashariki wamefika wakiwa na zawadi zao ambazo ni: dhahabu kujulisha kuwa huyu ni Mfalme, ubani kuwa huyu ni Kuhani na manemane kubashiri kifo. Mamajusi, kwa nyakati zile za kuzaliwa Yesu walikuwa ni watu wenye hekima na uwezo wa kutafsiri njozi ili kujua mambo yajayo…
Na Padre Joseph Luwela – Vatican. Papa Francisko amesema kwamba, tarehe 8 Desemba 2023 Mama Kanisa anaadhimisha Sherehe ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili. Bikira Maria aliamini katika pendo la Mungu na kutoa jibu la “Ndiyo” kwa upendo wa Mungu. Huu ni mwaliko kwa waamini na watu wote wenye mapenzi mema kujifunza kutoka kwa…
Na Padre Joseph Herman Luwela, – Vatican. Nyumba ya Baba yangu ni nyumba ya sala, toba na wongofu wa ndani na sio genge la biashara huria! Leo Kanisa linaadhimisha Dominika ya 3 ya Kipindi cha Kwaresima Mwaka B wa Kanisa. Himizo kubwa katika kipindi hiki cha Kwaresima ni toba na wongofu wa moyo na muunganiko…
Dominika ya Sita Ya Mwaka B wa Kanisa: Siku ya 32 ya Wagonjwa Ulimwenguni 2024 Maadhimisho ya Siku ya 32 ya Wagonjwa Ulimwenguni yananogeshwa na kauli mbiu “Si vizuri kwamba mwanadamu awe peke yake. Uponyaji wa wagonjwa katika kuponya mahusiano.” Baba Mtakatifu anaangalia vita kama gonjwa kubwa na la kutisha, uzee na upweke. Kumbe, kuna…
katika picha ni Masista wa , Jubilei ya miaka 25 ya Utawa kwa Masista wa Maria Mtakatifu Malkia wa Afrika (MMMMA), Jimbo Katoliki Sumbawanga. Adhimisho la Misa Takatifu limefanyika Parokia ya Epiphania Kanisa Kuu Jimboni humo. Jubilei ya miaka 50 Aliyeadhimisha Misa Takatifu ni Mhashamu, Damian Kyaruzi, Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki Sumbawan, na aliyepokea…