Mapokezi ya Mwadhama Polycarp Kardinal Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki Dsm, alipowasili Jimbo Katoliki Shinyanga katika ziara za kichungaji, mnamo tarehe 6.12.2023.
Katika picha ni baadhi ya waamini wa jimbo katoliki la Shinyanga wakiwa na nyuso za furaha wakimkaribisha Kardinali Pengo katika mipaka ya jimbo hilo
Mha Askofu Sangu aongoza mapokezi na kumkaribisha Mwadhama kadinali Pengo jimboni humo kwa ziara ya kichungaji kuanzia tar 06.12.2023
Na Padre Joseph Herman Luwela, – Vatican 06.Jan 2024 Mamajusi toka mashariki wamefika wakiwa na zawadi zao ambazo ni: dhahabu kujulisha kuwa huyu ni Mfalme, ubani kuwa huyu ni Kuhani na manemane kubashiri kifo. Mamajusi, kwa nyakati zile za kuzaliwa Yesu walikuwa ni watu wenye hekima na uwezo wa kutafsiri njozi ili kujua mambo yajayo…
Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa tarehe 5 Aprili 2024 amekutana na kuzungumza na Jumuiya ya Ndugu Wadogo wa La Verna na wale wanaotoka Kanda ya Toscana, kama sehemu ya kumbukizi ya miaka mia nane tangu Mtakatifu Francisko wa Assisi alipobahatika kupewa Madonda Mtakatifu mwilini mwake. Hii ilikuwa ni tarehe 15 Septemba 1224, yaani miaka miwili kabla…
Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu. Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu? Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako..”( Zaburi 42:1 – 3 )
Na. Pd Joseph Luwela-Vatican-Roma Utakatifu ni mchakato unaowawezesha waamini kuishi upendo katika utimilifu wake kadiri ya nguvu na mwanga wa Roho Mtakatifu. Maisha ya kila mwamini yawe ni kielelezo cha utume kutoka kwa Kristo Yesu anayetaka kuwaletea waja wake mabadiliko katika maisha, licha ya udhaifu na mapungufu yao ya kibinadamu, daima wakijitahidi kuambata upendo wa…
Usaili kwa kidato cha kwanza ni tarehe 3_4 January 2024 kutakuwa na mitihani. Kwa wanaohamia mitihani ya usaili ni December 2023 wazazi wa wahi nafasi ni chache, Asante kwa USHIRIKIANO wako, Mungu azidi kukubariki daima.
Sherehe ya Bikira Maria Kupashwa Habari kuwa atakuwa ni Mama wa Mungu kwa mwaka 2024 inaadhimishwa Jumatatu tarehe 8 Aprili 2024, baada ya tarehe 25 Machi 2024 kuangukia kwenye Juma Kuu. Tarehe 8 Aprili 2024 Mama Kanisa sehemu mbalimbali za dunia anaadhimisha Siku ya Kutetea Uhai na Utakatifu wa Maisha tangu pale mtoto anapotungwa mimba…