Tafakari Dominika 21 ya Mwaka B wa Kanisa: Imani, Matumaini na Utashi Kamili “Je nanyi pia mwataka kuondoka?”
Mwokozi wetu, katika Karamu ya mwisho, usiku ule alipotolewa, aliweka sadaka ya Ekaristi ya Mwili wake na Damu yake. Alifanya hivyo ili kuendeleza sadaka ya Msalaba siku zote mpaka atakaporudi, kusudi amwachie Bibi Arusi mpendwa, yaani Kanisa, ukumbusho wa kifo chake na ufufuko wake: Sakramenti ya upendo, umoja, kifungo cha mapendo, karamu ya Pasaka ambamo…