Sherehe ya Bikira Maria Kupashwa Habari ya Kuwa Mama wa Mungu
Sherehe ya Bikira Maria Kupashwa Habari kuwa atakuwa ni Mama wa Mungu kwa mwaka 2024 inaadhimishwa Jumatatu tarehe 8 Aprili 2024, baada ya tarehe 25 Machi 2024 kuangukia kwenye Juma Kuu. Tarehe 8 Aprili 2024 Mama Kanisa sehemu mbalimbali za dunia anaadhimisha Siku ya Kutetea Uhai na Utakatifu wa Maisha tangu pale mtoto anapotungwa mimba…