MASISTA WA MARIA MTAKATIFU MALKIA WA AFRIKA-SUMBAWANGA WAPATA WAPROFESI 16 WAPYA

Tarehe 07.12.2023 mwaka wa Bwana katika nyumba ya malezi parokia ya Chala

Katika picha ni Masista 16 wa nadhiri za kwanza wa shirika la Maria Mtakatifu Malkia wa Afrika-Jimbo la Sumbawanga 07.12,2023

Adhimisho la Misa Takatifu limefanyika katika Kanisa la Nyumba ya malezi ya Shirika hilo, iliyopo Parokia ya Mtakatifu Fransisco wa Sales – Chala Jimbo Katoliki Sumbawanga. Ikiwa ni utangulizi wa sherehe za Shirika hilo, ambazo hufanyika tarehe 08.12. au maarufu Nane Disemba Sherehe ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi(Emakulata).

Adhimisho la Misa Takatifu limeongozwa na Askofu Emeritus Damian Kyaruzi wa Jimbo la Sumbawanga, Na aliyepokea Nadhiri 16 za kwanza kwa Masista 16 ni Mama Mkuu wa Shirika hilo Mheshimiwa SR. Editruda Mbegu Mbele ya Mhashamu Baba Askofu Damian Kyaruzi, ambaye amemwakilisha askofu wa Jimbo Mha, Beatus Urassa ALCP/OSS.

Katika sherehe hizo za nadhiri za kwwanza wameudhuria , watu mbalimbali wakiwemo mapadri, watawa waamini wakinogeshwa na furaha ya walelewa amabo wameshuhudia safari ya dada zao ikifika mwisho katika hatua msingi ya nadhiri za awali tunawaombea udumifu mwema

Katika picha hapo chini ni mnadhiri mpya wa nadhiri za kwanza Sista Maria Nzunda kutoka parokia ya Tunduma jimbo katoliki Sumbawanga

SR MARIA Nzunda-MMMMA

Similar Posts

Leave a Reply