Mapokezi ya Mwadhama Polycarp Kardinal Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki Dsm, alipowasili Jimbo Katoliki Shinyanga katika ziara za kichungaji, mnamo tarehe 6.12.2023.
Katika picha ni baadhi ya waamini wa jimbo katoliki la Shinyanga wakiwa na nyuso za furaha wakimkaribisha Kardinali Pengo katika mipaka ya jimbo hilo
Mha Askofu Sangu aongoza mapokezi na kumkaribisha Mwadhama kadinali Pengo jimboni humo kwa ziara ya kichungaji kuanzia tar 06.12.2023
Na Padre Joseph Herman Luwela, – Vatican. Nyumba ya Baba yangu ni nyumba ya sala, toba na wongofu wa ndani na sio genge la biashara huria! Leo Kanisa linaadhimisha Dominika ya 3 ya Kipindi cha Kwaresima Mwaka B wa Kanisa. Himizo kubwa katika kipindi hiki cha Kwaresima ni toba na wongofu wa moyo na muunganiko…
Tarehe 07.12.2023 mwaka wa Bwana katika nyumba ya malezi parokia ya Chala Katika picha ni Masista 16 wa nadhiri za kwanza wa shirika la Maria Mtakatifu Malkia wa Afrika-Jimbo la Sumbawanga 07.12,2023 Adhimisho la Misa Takatifu limefanyika katika Kanisa la Nyumba ya malezi ya Shirika hilo, iliyopo Parokia ya Mtakatifu Fransisco wa Sales – Chala…
Sherehe ya Bikira Maria Kupashwa Habari kuwa atakuwa ni Mama wa Mungu kwa mwaka 2024 inaadhimishwa Jumatatu tarehe 8 Aprili 2024, baada ya tarehe 25 Machi 2024 kuangukia kwenye Juma Kuu. Tarehe 8 Aprili 2024 Mama Kanisa sehemu mbalimbali za dunia anaadhimisha Siku ya Kutetea Uhai na Utakatifu wa Maisha tangu pale mtoto anapotungwa mimba…
Kipindi cha Kwaresima ni fursa ya kuamsha na kupyaisha ari na mwamko wa kimisionari, tayari kujisadaka bila ya kujibakiza kwa ajili ya kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu hadi miisho ya dunia. Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waamini kuwakumbuka na kuwaombea wainjilishaji wote, ili waweze kuwa ni vyombo na mashuhuda wa kile wanacho amini, kufundisha…
Na Padre Joseph Herman Luwela, – Vatican 06.Jan 2024 Mamajusi toka mashariki wamefika wakiwa na zawadi zao ambazo ni: dhahabu kujulisha kuwa huyu ni Mfalme, ubani kuwa huyu ni Kuhani na manemane kubashiri kifo. Mamajusi, kwa nyakati zile za kuzaliwa Yesu walikuwa ni watu wenye hekima na uwezo wa kutafsiri njozi ili kujua mambo yajayo…
katika picha ni Masista wa , Jubilei ya miaka 25 ya Utawa kwa Masista wa Maria Mtakatifu Malkia wa Afrika (MMMMA), Jimbo Katoliki Sumbawanga. Adhimisho la Misa Takatifu limefanyika Parokia ya Epiphania Kanisa Kuu Jimboni humo. Jubilei ya miaka 50 Aliyeadhimisha Misa Takatifu ni Mhashamu, Damian Kyaruzi, Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki Sumbawan, na aliyepokea…