Tarehe 07.12.2023 mwaka wa Bwana katika nyumba ya malezi parokia ya Chala
Katika picha ni Masista 16 wa nadhiri za kwanza wa shirika la Maria Mtakatifu Malkia wa Afrika-Jimbo la Sumbawanga 07.12,2023
Adhimisho la Misa Takatifu limefanyika katika Kanisa la Nyumba ya malezi ya Shirika hilo, iliyopo Parokia ya Mtakatifu Fransisco wa Sales – Chala Jimbo Katoliki Sumbawanga. Ikiwa ni utangulizi wa sherehe za Shirika hilo, ambazo hufanyika tarehe 08.12. au maarufu Nane Disemba Sherehe ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi(Emakulata).
Adhimisho la Misa Takatifu limeongozwa na Askofu Emeritus Damian Kyaruzi wa Jimbo la Sumbawanga, Na aliyepokea Nadhiri 16 za kwanza kwa Masista 16 ni Mama Mkuu wa Shirika hilo Mheshimiwa SR. Editruda Mbegu Mbele ya Mhashamu Baba Askofu Damian Kyaruzi, ambaye amemwakilisha askofu wa Jimbo Mha, Beatus Urassa ALCP/OSS.
Katika sherehe hizo za nadhiri za kwwanza wameudhuria , watu mbalimbali wakiwemo mapadri, watawa waamini wakinogeshwa na furaha ya walelewa amabo wameshuhudia safari ya dada zao ikifika mwisho katika hatua msingi ya nadhiri za awali tunawaombea udumifu mwema
Katika picha hapo chini ni mnadhiri mpya wa nadhiri za kwanza Sista Maria Nzunda kutoka parokia ya Tunduma jimbo katoliki Sumbawanga
katika picha ni Masista wa , Jubilei ya miaka 25 ya Utawa kwa Masista wa Maria Mtakatifu Malkia wa Afrika (MMMMA), Jimbo Katoliki Sumbawanga. Adhimisho la Misa Takatifu limefanyika Parokia ya Epiphania Kanisa Kuu Jimboni humo. Jubilei ya miaka 50 Aliyeadhimisha Misa Takatifu ni Mhashamu, Damian Kyaruzi, Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki Sumbawan, na aliyepokea…
Mama Kanisa katika masomo ya dominika hii anatukumbusha kuwa kwa Sakramenti ya Ubatizo na kipaimara sisi sote tumeitwa kuihuburi Injili kwa kuishi ukristo wetu vyema sio kwa sheria za maumbile bali kwa kuwa viumbe vipya ndani ya Kristo na kuona fahari juu ya Msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo ambao kwao tumekombolewa. Hii ni changamoto…
Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu. Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu? Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako..”( Zaburi 42:1 – 3 )
Na Padre Joseph Herman Luwela, – Vatican 06.Jan 2024 Mamajusi toka mashariki wamefika wakiwa na zawadi zao ambazo ni: dhahabu kujulisha kuwa huyu ni Mfalme, ubani kuwa huyu ni Kuhani na manemane kubashiri kifo. Mamajusi, kwa nyakati zile za kuzaliwa Yesu walikuwa ni watu wenye hekima na uwezo wa kutafsiri njozi ili kujua mambo yajayo…
Mapokezi ya Mwadhama Polycarp Kardinal Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki Dsm, alipowasili Jimbo Katoliki Shinyanga katika ziara za kichungaji, mnamo tarehe 6.12.2023. Katika picha ni baadhi ya waamini wa jimbo katoliki la Shinyanga wakiwa na nyuso za furaha wakimkaribisha Kardinali Pengo katika mipaka ya jimbo hilo
Usaili kwa kidato cha kwanza ni tarehe 3_4 January 2024 kutakuwa na mitihani. Kwa wanaohamia mitihani ya usaili ni December 2023 wazazi wa wahi nafasi ni chache, Asante kwa USHIRIKIANO wako, Mungu azidi kukubariki daima.